Swahili transcript

Halafu wanahoji kwa nini asilimia 97?

Kwa nini isiwe?

Waswahili wanasema paukwa, pakawa. Wao hawakuwepo.

wale 16 waliokuwepo ni wadogo sana. Wao ambao

wangetingisha CCM hawakuwepo. Hakukuwa CHADEMA,

hakukuwa ACT ndio ambao tungekwenda nao. sisi

tulijitayarisha kwamba tunakwenda kupambana

vyama vyenzetu vikubwa. Hawakuwepo. Mwananchi

afanyeje?

Twataka kuwaambia hata hawa wafuasi wao walipigia

Chama cha Mapinduzi. Walipigia Chama cha Mapinduzi.

Wale wanaohoji kwa nini asilimia 97, hiyo ndio

kilichotokea. Ni asilimia 97 ya waliopiga kura,

sio ya Watanzania wote. Ya waliopiga kura ni

asilimia 97. Kazi imefanyika, kampeni imefanyika,

watu wameelewa, wamepiga kura. Mungu ni mkubwa,

kwamba lile balaa lao walilianza saa tano sijui

sita, watu walishajipeleka mapema asubuhi. Wakapiga

kura wakaondoka. Mungu ni mkubwa. Hasa kwenye

miji, hawakufanya kote hasa kwenye miji. Kwa

hiyo ndugu zangu, sisi ni Watanzania. Tanzania

itajengwa Watanzania. Jeraha limetokea, lazima

sisi Watanzania tutibu jeraha letu.

End of transcript · 140 words

iPhone app Translate videos on your iPhone Paste a TikTok, Instagram or X link, add subtitles in your language and save the video to Photos.

Read any video in your language

Paste a link from X, TikTok, YouTube or Instagram. You get a page like this one.

© 2026 TranslateMom Transcripts Sources Pricing Legal